Mwaka 2013 kwenye airport ya LAX Kanye West alihusishwa na fujo ambapo alimshambulia paparazi mmoja aliyekuwa akijaribu kumpiga picha Kanye West.
Fujo hizi zilinaswa kwenye camera mbalimbali za mapaparazi waliokua karibu na tukio hilo na kuanza kusambaa kwenye mitandao.
Kutokana na tukio hilo kufika mahakamani, hivi sasa Kanye West amehukumiwa miaka 2 ya probation na masaa 250 ya kufanya kazi za jamii.
Zaidi ya hapo Kanye anatakiwa kuhudhuria session 24 za program ya anger management. Kanye West alikubaliana na hayo yote ili kumalizana na kesi hiyo hapo mahakamani.
[youtube youtubeurl=”p3nW2Kh-yfc” ][/youtube]