Leo April 13 2019 club ya Simba SC imehitimisha safari yake ya kucheza mchezo wa marudiano wa robo fainali ya CAF Champions League dhidi ya TP Mazembe, Simba ilienda kucheza mchezo wa marudiano baada ya mchezo wa kwanza Dar es Salaam kumalizika kwa Simba SC kupata sare tasa (0-0).
Simba ilienda Lubumbashi kutafuta sare ya magoli au ushindi ambao ungewawezesha kusonga mbele lakini mambo yameendelea kwenda mlama kwa Simba SC katika game zake za ugenini, Simba kuanzia hatua ya makundi hadi robo fainali hakuwahi kupata ushindi wala sare ugenini.
TP Mazembe wamedhihirisha ubora wao kwa Simba kwa kuifunga magoli 4-1, magoli ya TP Mazembe yakifungwa na Chongo dakika ya 23, Elia dakika ya 38, Tresor Mputu dakika ya 62 na Muleka dakika ya 75, hiyo ni baada ya Simba SC kupata goli la mapema dakika ya 2 kupitia kwa Emmanuel Okwi na hilo kuwa ndio goli pekee la Simba kufunga ugenini CAF Champions League kuanzia hatua ya makundi
Simba SC baada ya kufanikiwa kumudu kucheza game zake za nyumbani na kupata matokeo yanayoridhisha, sasa watatakiwa kujifunza kucheza game za ugenini pia kwa maana wamekuwa hawana matokeo mazuri katika michuano ya CAF Champions League msimu wa 2018/2019 katika mechi za ugenini.
Rais Karia kaiomba kamati ya RC Paul Makonda kuhamishia nguvu kwa Serengeti Boys