Kampuni ya SportPesa ambao ndio wadhamini wakuu wa timu za Simba SC na Yanga wametangaza ujio wa club ya Sevilla ya nchini Hispania kuja Tanzania, ujio wa club hiyo unakuja Tanzania kucheza kati ya Simba SC na Yanga ambao wanadhaminiwa na kampuni hiyo.
Sevilla ambao ndio Mabingwa mara tano wa Kombe la UEFA Europa League, mwanzo ilikuwa waje Tanzania kucheza mchezo wa kirafiki na timu ambayo ingeundwa kwa pamoja kwa kuleta uzalendo kwa kuwaunganisha wachezaji wa Simba na Yanga halafu kuunda timu moja, ila moja kati ya timu hizo mbili ilikataa wazo la kuungana.
“Tukishirikiana na LaLiga na sisi SportPesa tunaleta timu ambayo imewahi kuwa Mabingwa LaLiga vile vile imewahi kuwa mara tano Mabingwa wa Europa League, hiyo timu inaitwa Sevilla FC, ujio wao watakuja kucheza na timu moja ya Tanzania kiu yetu namba moja ilikuwa kwa bahati mbaya haikukubalika ilikuwa kumpa sapoti Mh Rais Magufuli kwa kuondoa uhasama katika mpira Simba na Yanga ziungane katika hii mechi lakini moja kati ya hizi timu ilikataa”>>> Tarimba Abbas
Sevilla watacheza Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kati ya Simba SC au Yanga wakati huu, wadhamini wao wakuu wakiamua ni njia ipi itakayotumika kwa timu moja wapo kati ya hizo kukata tiketi ya kucheza na Sevillla ila kumuunga mkono Rais Magufuli na kuleta uzalendo wazo lao la kwanza ilikuwa ni timu hizo ziungane.
Mwana FA kakutana na Jose Mourinho uso kwa uso, kamwambia yale maneno yake?