Fahamu kuwa ni siku 18 zimepita tangu kifo cha rapper Nipsey Hussle kitokee alifariki March 31,2019 mjini Los Angeles nje ya duka lake ‘The Marathon Clothing Store’ , mashabiki wengi wameibeba kauli kubwa ya ‘The Marathon Continues” na wengi kuahidi kuutekeleza.
Kikubwa ambacho kimeripotiwa na mitandao mingi Marekani ni kuwa duka la nguo la “The Marathon Clothing Store” limepokea oda za nguo mtandaoni za dola za Kimarekani milioni 2 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 4 za Kitanzania kwa muda mfupi tokea Nipsey Hussle afariki dunia.
Rapper Nipsey Hussle alipumzishwa April 12,2019 katika makaburi ya Forest Lawn Memorial Park yaliyopo Hollywood Hills na mpaka sasa mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji hayo ameshafikishwa Mahakamani na kufunguliwa shtaka la mauaji.
AUDIO: Ulipitwa na mwigizaji Irene Uwoya atema cheche “Kuna watu nikuwafungia vioo tu”, Bonyeza PLAY hapa chini kusikiliza.