Taifa la Burundi limepata pigo ikiwa zimebaki wiki kadhaa kabla ya timu yao ya taifa ya Burundi kuishuhudia kwa mara ya kwanza ikicheza fainali za mataifa ya Afrika nchini Misri, Burundi leo imempoteza kiungo wake mahiri Papy Faty aliyefariki kwa matatizo ya moyo.
Staa huyo wa zamani wa club ya Bidvest ya Afrika Kusini umauti umemkuta akiwa na timu yake ya Malanti Chiefs ya Swaziland ikipambana na timu ya Green Mamba katika uwanja wa Killarney ulio nje kidogo ya mji wa Mbabane ila Papy Faty ambaye alikuwa na tatizo la moyo kwa muda mrefu alianguka uwanjani na kupoteza maisha.
Papy Faty umauti unamkuta ikiwa ni miaka mitatu imepita toka madaktari wamshauri kuwa aachane na kucheza soka, kutokana na kubainika kuwa na tatizo la moyo, hivyo hiyo ilikuwa ni hatari kwa maisha yake, Papy mwenye umri wa miaka 28 umauti umemkuta baada ya kuanguka uwanjani dakika ya 15 na kukimbizwa hospitali walipothibitisha kuwa amepoteza maisha.
Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23