Tunayo stori kutokea kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Edwin Mhede ambapo ametoa wito kwa Wenye viwanda na wawekezaji nchini kusajili alama za bidhaa zao ili ziweze kulindwa ziwapo sokoni.
Dk.Mhende amesisitiza wamiliki wa Viwanda na Wafanyabiashara, washirikiane na Tume ya Ushindani Katika kupambana na Bidhaa Bandia, huku akiwataka watumie fursa ya uwepo wa Tume ya Ushindani ili kuhakikisha kuwa ‘brands’ zao zinalindwa.