Rais Magufuli ameuagiza Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Mbeya kumgharimia matibabu Mtoto aliyelawitiwa, ambaye Mama yake Mzazi alipambana na Walinzi wa Rais, ili kumueleza hali ya Mtoto wake huyo, katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya.