Timu za England zina nafasi ya kuandika historia kwa kuwa ligi ya kwanza Ulaya kuingiza vilabu vinne kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa na Europa, Liverpool na Tottenham Hotspur bado ziko kwenye UEFA Champions League, wakati leo Alhamisi hii Arsenal na Chelsea zinacheza na Valencia na Eintracht Frankfurt kwenye nusu fainali ya Europa League.
Arsenal wamepoteza michezo mitatu mfululizo kwenye Ligi Kuu ya England, kipigo cha mwisho walikipata dhidi ya Leicester kwa mabao 3-0 walipotembelea dimba la King Power. Kipigo hicho kimefifisha matumaini ya Arsenal kumaliza katika nafasi nne za juu ili kuweza kushiriki ligi ya Mabingwa Ulaya.
Matumaini yao ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao ni kushinda Europa pekee. Wanacheza dhidi ya Valencia dimbani Emirates katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali huku Valencia wakiwa katika nafasi ya uhakika kushiriki ligi ya mabingwa msimu ujao.
Kocha wa Arsenal Unai Emery alisema walijisikia vibaya kupoteza dhidi ya Crystal Palace, Wolves na Leiceste City “Lakini tunahitaji kuendelea. Tuna ligi mbili ambazo bado tunahitajika kucheza vizuri ligi ya Uingereza na Europa. Zote hizi zina nafasi ya kutufikisha kwenye ligi ya mabingwa ambalo ndio lengo letu.
Chelsea ni timu ambayo imenufaika na kiwango kibovu cha Arsenal, hivyo wameweza kujiimarisha katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi – wao watacheza dhidi ya Eiintracht Frankurt.
Timu hiyo kutoka ligi ya Bundesliga sio ya kupuuzwa, ushindi wao dhidi ya Inter Milan na Benfica kwenye hatua zilizopita inaonyesha jinsi gani walivyo wazuri. Ikiwa ndiyo timu pekee kutoka Bundelsiga katika mashindano ya Ulaya, matumaini yote ya Ujerumani yapo mabegani mwao hivyo Chelsea watakuwa na kazi ya ziada kuwatoa.
Chesea wanacheza mchezo huu baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Manchester United Jumapili iliyopita. Eden Hazard anasema yeye pamoja na wachezaji wenzake wataingia katika mchezo huo wakiwa na kujiamini zaidi baada ya mchezo wa Man United, game za leo zitaonesha ST World Football.
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania