Matumaini ya mashabiki wa club ya Dar es Salaam Young Africa kuiona timu yao ikishiriki michuano ya kimataifa msimu wa 2019/202o inazidi kufutika, hiyo inatokana na club yao kuruhusu kufungwa magoli 2-0 dhidi ya Lipuli FC katika uwanja wa Samora Iringa mchezo huo ukiwa wa nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup.
Magoli ya Lipuli FC yaliohitimisha safari ya Yanga katika michuano ya Azam Sports Federation Cup yalifungwa na mchezaji wao wa zamani Paul Nonga dakika ya 28 na Saliboko dakika ya 38, hadi dakika 90 zinamalizika Yanga walishindwa kupindua matokeo na kujikuta wakitupwa nje ya michuano hiyo.
Baada ya ushindi huo Lipuli FC watacheza mchezo wa fainali dhidi ya Azam FC ambayo nayo ilitangulia mapema fainali kwa kuifunga KMC 1-0, ndoto ya Yanga kucheza michuano ya kimataifa inayoandaliwa na CAF imeishia hapa maana Bingwa wa michuano ASFC ndio anapata nafasi ya kucheza katika michuano ya Kombe la shirikisho Afrika.
Wakati kwa upande wa CAF Champions League wanakuwa na nafasi ndogo zaidi kutokana na sasa kuongoza Ligi akiwa ameizidi Simba SC michezo 4, anaongoza Ligi kwa kuwa na point 80 wakati Simba ana point 78 na michezo minne ya viporo, hivyo nafasi ya Yanga kuwa Bingwa Ligi Kuu na kupata tiketi ya kushiriki CAF Champions League 2019/20 ni ndogo.
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania