Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga Yono Stanley Kivella pamoja na kuwa kura hazikutosha kumuwezesha kuwa mshindi, ameonesha dhamira ya dhati ya kuunga mkono uongozi mpya wa Yanga SC uliyochaguliwa kwa ajili ye kuiongoza club hiyo.
Yanga SC siku ya Jumapili ya May 5 2019 ilifanya uchaguzi mkuu na kufanikiwa kumpata Mwenyekiti mpya Mshindo Msolla na makamu ni Fredrick Mwakalebela, baada ya kumalizika uchaguzi huo wanachama wa Yanga walikubaliana kwa pamoja kuvunja kambi zao na kuwaunga mkono viongozi.
Yono Stanley Kivella ambaye alikuwa mgombea makamu mwenyekiti wa Yanga ameonesha ukomavu wa kidemokrasia kwa kuvunja makundi na kuamua kuichangia Yanga Tsh milioni 20 ili zisaidie club hiyo huku akimkabidhi pesa hizo aliyekuwa mshindani wake katika uchaguzi Fedrick Mwakalebela ambaye ni makamu mwenyekiti mpya wa Yanga SC.
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania