Leo Mei 14, 2019 Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa ripoti ya mwaka iliyojikita kuhusu hali ya Haki za Binadamu hasa kwa mambo chanya na yaliyoathiri ambapo kwa mwaka 2018 imejikita katika Ukatili wa Kingono kwa Watoto.
Akizungumzia ripoti hiyo, Afisa utafiti wa LHRC, Fundikila Wazambi amesema wameangalia haki ya kuishi ikiwemo mauaji kwa njia ya kishirikina, ajali za barabarani ambapo kwa imani za kishirikina mikoa ya Tabora na Shinyanga ikiongoza, huku mauaji dhidi ya Wazee yakiongezeka ambapo watoto wanawauwa Wazazi wao kwa ajili ya kuhitaji mali.