Kocha ni moja kati ya viungo muhimu katika timu ili ifanye vizuri na mara nyingi ikitokea timu ikawa inafanya vibaya, uongozi wa juu mtu wa kwanza kumuadhibu huwa ni kocha na sio mchezaji, club ya KRC Genk ambao ndio Mabingwa wa Ligi Kuu ya Ubelgiji msimu wa 2018/2019 wamepata pigo kwa kocha wao Philippe Clement kutangaza kuwa anaondoka.
Philippe Clement mwenye umri wa miaka 45 aliyewasaidia KRC Genk kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza baada ya miaka nane, ametangaza kuondoka katika club hiyo na kwenda kujiunga na Club Brugge ambao ni wapinzani wa karibu wa Genk katika mbio za kuwania Ubingwa msimu ulioisha Brugge akimaliza nafasi ya pili.
Kocha huyo ametangaza kufikia maamuzi ya kuondoka kwa ajili ya kwenda kutafuta changamoto mpya ila ameamua kurudi katika club ambaye amewahi kuichezea kwa miaka 10 (1999-2009), amewahi kuitumikia katika nafasi ya uscout, kocha wa muda na kocha msaidizi kwa vipindi tofauti tofauti, hivyo anarudi baada ya kudumu Genk kwa miaka miwili (2017-2019).
Clement alijiunga na Genk December 18 2017 akitokea Beveren kama kocha mkuu na kuisaidia club hiyo kumaliza msimu wakipata tiketi ya kucheza Europa League, kabla ya msimu huu kuipa Ubingwa na kupata nafasi ya kucheza UEFA Champions League msimu wa 2019/2020, KRC Genk ni club inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta.
EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega