Kamati Kuu ya ACT Wazalendo imesema ipanga kuimarisha ushirikiano kati yao na Vyama vingine vya Upinzani nchini katika kuipigania, kuitetea na kuilinda misingi ya Kidemokrasia ambayo imevurugwa kwa kiasi kikubwa.
Hayo yameelezwa leo na Kiongozi wa Chama hicho Zitto Kabwe alipokuwa akiwasilisha maazimio ya kamati hiyo leo June 11, 2019 katika Ofisi Ndogo ya Chama hicho Magomeni jijini DSM, ambapo amesema kuwa wamepanga kujadili namna Vyama vya Upinzani vitakavyoshirikiana katika uchaguzi ujao.
“Kamati Kuu imewaagiza Viongozi Wakuu Wakuu wa Chama kuendelea kushiriki kikamilifu kwenye ushirikiano na vyama vingine na pia kuhakikisha utekelezaji thabiti wa Azimio la Zanzibar lililoutangaza mwaka huu kuwa mwaka wa mapambano ya kudai Demokrasia” Zitto Kabwe
“Pia Kamati Kuu imemuagiza Katibu Mkuu wa Chama kuwaandikia Makatibu Wakuu wa Vyama vyote tunavyoshirikiana navyo kuitisha kikao cha Viongozi Wakuu kutafakari namna bora ya Vyama vya Upinzani kushirikiana kwenye uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika October mwaka huu,” Zitto Kabwe