Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango leo June 13, 2019 amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019-2020 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nimekusogezea mambo kumi ambayo hayakutarajiwa katika Bajeti iliyosomwa.
“Serikali imeanzisha kitengo kipya cha kupokea malalamiko ya kodi na kitaratibiwa na Wizara ya Fedha na Mipango, kitahusisha kupokea malalamiko kutoka kwa walipa kodi yakiwamo ya kuombwa rushwa na Watumishi wa Mamlaka ya Kodi TRA” Waziri Mpango
“Wananchi wataruhusiwa kutoa mizigo yao bandari bila ulazima wa kutumia Mawakala ili kupunguza gharama kwa wananchi, lakini mizigo inayokwenda nje itaendelea kuhudumiwa na Wakala” Waziri Mpango
“Napendekeza kufutwa kwa ada ya matumizi ya maji kwa watumiaji wenye visima nyumbani ambayo ilikuwa inatozwa kuanzia Shilingi 100,000 na kuendelea kulingana na matumizi ya maji” Waziri Mpango
‘Tozo zote zilizokuwa zinatozwa kwa Dola za Kimarekani zitatozwa kwa Shilingi ya Tanzania, isipokuwa kwa shehena za kemikali zinazokwenda nje ya nchi” Waziri Mpango
“Kufuatia mkutano wa Rais Magufuli na Wafanyabiashara uliofanyika Ikulu DSM, tumeazimia kufuta ada na tozo 54 zinazotozwa na Idara na Taasisi za fedha zinazojitegemea ili kuondoa kero kwa Wafanyabiashara” Waziri Mpango
“Napendekeza kuongeza muda wa leseni ya udereva kutoka miaka 3 hadi 5, kuongeza tozo ya leseni 40000 hadi 70000, ada ya usajili wa magari 10000 hadi 50000, bajaji kutoka 10000 hadi 30000 na pikipiki kutoka 10000 hadi 20000” Waziri Mpango
“Kufuta kwa msamaha kodi ya ongezeko la thamani kwenye taulo za kike kwa kuwa haujawezesha kupatikana kwa bei nafuu kwa bidhaa hiyo muhimu kwa walengwa, badala yake ni kuwanufainisha Wafanyabiashara” Waziri Mpango
“Serikali itapunguza kiwango cha kodi kwa umeme unaouzwa kutoka Tanzania kwenda Zanzibar kutoka kwa asilimia 18, hadi 0 ili kuwapunguzia gharama za maisha kwa wananchi wa Zanzibar” Waziri Mpango
“Napenda kuwasisitiza tena watumishi wa TRA kwamba hairuhusiwi kufunga biashara ili kushinikiza Mfanyabiashara alipe kodi au malimbikizo ya kodi isipokuwa kwa kibali cha Kamishna Mkuu wa TRA” Waziri Mpango
“Kati ya kipindi cha July 2018 na April 2019 Serikali imetumia Bilioni 232.8 kununua ndege kwa ajili ya Shirika la Air Tanzania, ambapo ndege za Boeing 787-8 Dreamliner na Bombadier Q400 zitawasili nchini mwishoni mwa mwaka huu 2019″ Waziri Mpango
“Napendekeza kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye nywele za bandia zinazotengenezwa nchini na asilimia 25 kwenye nywele bandia zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, lengo la hatua hii ni kuongeza mapato ya Serikali” Waziri Mpango
LIVE: WAZIRI MPANGO AKIWASILISHA BAJETI YA SERIKALI 2019/2020 BUNGENI – DODOMA