Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

CEO wa Simba SC athibitisha kuwa ana miezi miwili tu Simba SC

on

Baada ya uwepo wa tetesi za chini kwa chini kuwa CEO wa Simba SC Crescentius Magori yupo mbioni kuondoka na nafasi hiyo kutaka kuchukuliwa na kiongozi mwingine kutoka nje ya nchi, leo June 13 2019 amethibitisha kuwa ataondoka mkataba wake umemalizika.

Magori anaondoka Simba SC akiwa ameitumikia timu hiyo kwa miezi sita na hadi amalize muda wa uongozi wake ukijumlisha miezi miwili atakayoongeza, kipindi wanasubiria mtendaji mkuu mpya atakuwa ameweka rekodi ya kuwa mtendaji mkuu wa kwanza wa Simba SC toka timu hiyo iingie katika mfumo wa mabadiliko.

.
“Mkataba wangu wa miezi sita umemalizika, baada ya kuombwa na Bodi ya Wakurugenzi nimeamua kutumikia kwa miezi miwili zaidi wakati klabu ikiendelea kutafuta Mtendaji Mkuu mwengine atakayechukua nafasi yangu”>>> Crescentius Magori

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments