Baada ya aliyekuwa golikipa wa Yanga SC Beno Kakolanya kudaiwa kuwa katika mahusiano mabovu na kocha wake Mwinyi Zahera, hatimae Kakolanya amehamia rasmi upande wa pili na kumaliza uvumi uliokuwa ukiendelea kwa muda mrefu kuwa anatakiwa na Simba SC.
Simba SC imetangaza rasmi kuwa imeingia mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Simba SC, hivyo tutarajie kumuona Beno Kakolanya ndani ya jezi nyekundu ya Simba SC kwa maana hiyo sasa ushindani wa namba Simba SC katika eneo la magolikipa utakuwa mkubwa kwa golikipa namba moja wa Simba SC Aishi Manula.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Beno Kakolanya aliyejiunga na Simba SC, aliingia katika mvutano na kocha wake wa Yanga SC Mwinyi Zahera baada ya kugoma na kutaka kushinikiza alipwe pesa zake anazodai ndio arudi kufanya mazoezi na timu hiyo na kuendelea kuitumikia katika mechi.
EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega