Serikal kupitia wizara ya Afya imetangaza kujenga hospitali ya rufaa ya kikanda mkoani Geita ili kupunguza msongamano katika hospital ya rufaa ya kanda ya Mwanza, Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu amesema kanda ya ziwa inakadiriwa kuwa na watu million 13.4
“Hospitali hii lazima tuvutie wagonjwa kutoka Kongo,Burundi na Rwanda na tunataka kuifanya Geita Kuwa kituo cha Utalii wa matibabu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania” >>>Waziri Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu ameiagiza mikoa na halmashauri kuhakikisha zinaunda kamati za ulinzi kwa wanawake na watoto katika ngazi za kata na vijiji ili kuimarisha ulinzi na usalama kwa makundi hayo
Ummy ametoa maagizo hayo katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika mkoani Geita alipokuwa akitoa takwimu ya matukio ya ukatili kwa watoto” katika kila watoto wa kike 100 watoto 20 wanapata ujauzito kabla ya miaka 18″ UMMY MWALIMU
LIVE MAGAZETI: Ubakaji watoto watisha, Undani siku 17 kitanzi cha mifuko ya plastiki