Rais wa zamani wa chama cha soka Ulaya UEFA Michel Platini amejikuta katika wakati mgumu kufuatia kushikiliwa na kuhojiwa kwa tuhuma za rushwa nchini Ufaransa, Platini alijiuzulu nafasi yake ya Urais wa UEFA kwa tuhuma za rushwa.
Uchunguzi unaondelea na uliomfanya Platini akamatwe unahusiana nafasi ya kupewa uenyeji Qatar wa Kombe la dunia 2022, kitu ambacho kinahisiwa kuwa kilipitishwa kwa rusha na sio halali, hivyo Platini ni miongoni wa wanaotuhumiwa kwa rushwa katika sakata hilo.
Platini aliondoka kwa kashfa katika nafasi ya Urais wa UEFA 2015 baada ya kudumu katika nafasi hiyo kwa miaka nane toka 2007, Platini ambaye alifungiwa na FIFA kwa tuhuma za rushwa anatuhumiwa kuhusika kwa karibuni kushawishi Qatar kupewa uenyeji wa Kombe la dunia maamuzi ambayo yalifanyika 2010,w
EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega