Rais Magufuli amemruhusu Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda kwenda Misri kwenye michuano ya (AFCON), kuihamasisha Taifa Stars baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kumuomba ruhusa wakiwa kwenye uzinduzi wa Ghala na Mitambo ya Taifa Gas unaofanyika Kigamboini.
“Makonda umesema ukienda Misri Taifa Stars tutashinda kutokana na motisha ya ushangiliaji, panda ndege nenda si umesema tutashinda nenda” Rais Magufuli
“Mwanzo wa Taifa Stars sio mbaya kwanza wamefungwa tugoli tuwili tu na timu kubwa kama ile nina imani watafanya vizuri” Rais Magufuli