Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Rapper kutokea kundi la Migos Offset pamoja na mke wake Cardi B wanampango wa kumfanyia mtoto wao Kulture sherehe ya kutimizia mwaka mmoja itakayogharimu kiasi cha dola za Kimarekani 400,000 sawa na zaidi ya Tsh Mil.900
Inaelezwa kuwa Kulture anatimiza mwaka mmoja Julai 10 mwaka huu 2019 na kutajwa kuwa zawadi itakayotolewa kutoka kwa Cardi B na Offset ni vito vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 2o0 za Kitanzania ambapo sonara Eliantte ndio ametajwa kuandaa vito hivyo.
Kupitia Insta Live ya Cardi B aliwahi kufunguka na kusema kuwa hii ndio sherehe ya kuzaliwa ya kwanza ya mtoto wake hivyo anataka kuifanya kuwa ya kipekee. Inaelezwa kuwa Cardi B aliwahi kumnunulia mtoto wake bangili yenye thamani zaidi ya Mil.100 za kitanzania.
VIDEO: ULIPITWA NA HII YA MISS KINONDONI 2019 “HATUANGALII UZURI, TUNAANGALIA HESHIMA”?