Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka saba Mkazi wa Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma amelawitiwa na Mtu mzima amabaye hajafahamika kisha kumuwekea udongo katika sehemu ya haja kubwa.
Mtoto alielawitiwa amesema kuwa Mtu huyo alikuwa akimfunga kitambaa machoni wakati akitekeleza kitendo hicho katika kichaka na kumwambia kuwa asiseme kwa mtu yoyote na pia anaeleza kuwa alishindwa kumwambia Mama yake kwa kugopa kupigwa.
Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma tayari limeanza kufanya uchunguzi ili kuweza kumbaini na kumkamata Mtuhumiwa wa tukio hilo ambaye hadi sasa hajajulikana huku mtoto huyo akidai kuwa akimuona mtu huyo anaweza kumtambua.