Mbunge wa Jimbo la Starehe nchini Kenya Charles Kanyi maarafu kama Jaguar amekamwatwa leo June 25,2019 nchini humo kutokana na kauli yake aliyoiongea siku kadhaa zilizopita kuhusu kuwataka wafanyabiashara kutokea Nchi tofauti ikiwemo Tanzania kurudi kwao.
Kauli hiyo imeonekana kupigwa vita na watu wengi ikiwemo Watanzania ambapo wengi wanaamini kuwa Kenya na Tanzania ni nchi zenye urafiki mkubwa na hivyo Mbunge huo hakutakiwa kutoa kauli hiyo. Mastaa mbalimbali wametoa maoni yao kuhusu kauli hiyo akiwemo Mwimbaji Ben Pol ambaye amepost video kupitia ukurasa wake wa instagram akiimba ‘Kwetu Pazuri’
“My brother @jaguarkenya sijui nianzie wapi lakini matamshi yako ya jana hayakuleta shangwe kamwe. Maana ya kiongozi ni kuwaongoza watu wako kwa njia mwafaka na sio vita au uchonganishi hasa hasa kwa majirani zetu Tanzania na Uganda”
“Sisi wote tunatafuta riziki duniani ili tuweze kulisha familia zetu na kujenga nchi yetu. Kuna wakenya wanatafuta riziki kwa nchi zingine mbali na Kenya so uamuzi wako wa kuipa serikali masaa ishirini na nne kuwatoa wafanyikazi wenye biashara zao ambao sio wakenya ulichemsha. Anyway nakuombea Mungu akupe nguvu ili uweze kuwa kiongozi wa maendeleo” >>>aliandika Prezzo
VIDEO: UGONJWA ULIVYOMBADILISHA KUWA KAMA ‘NYANI’, HAUTIBIKI