Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Daktari feki ajulikanaye kwa jina la Abdallah Bushiri (42) mkazi wa Igodima Jijini Mbeya kwa tuhuma za kufanya kazi ya utabibu kwa kutibu magonjwa ya wanawake bila kuwa na Taaluma ya Udaktari.
Akizungumza na AyoTV katika Kituo cha Polisi Kati, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ulrich Matei amesema mtuhumiwa alikamatwa June 24 mwaka huu nyumbani kwake.
Amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa kufuatia baadhi ya wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi hilo kuhusu shughuli anazofanya Daktari huyo na akawekewa mtego uliowezesha kukamatwa na kupekuliwa nyumbani kwake.
Kamanda Matei amesema baada ya kupekuliwa nyumbani kwake, Daktari huyo feki alikutwa na vifaa tiba pamoja na dawa mbalimbali ambazo zinamilikiwa na Serikali zikiwa na nembo ya Bohari ya Dawa (MSD) pamoja na nembo inayoonyesha kuwa ni mali ya Serikali.
RC NA KAMANDA WAKESHA WAKIHESABAU MADINI YALIYOKAMATWA NA MBWA YA BILIONI KASORO