Mbio za kuwania uteuzi wa kupeperusha bendera ya Chama cha Democratic katika uchaguzi wa mwakani nchini Marekani zimeshika kasi, ambapo wagombea 10 kati ya ishirini wameshindana katika mdahalo wa TV.
Wagombea 10 kati ya 20 wamechuana usiku wa kuamkia leo June 27, 2019 katika mdahalo wa TV ambao ulitazamwa na mamilioni ya raia wa Marekani ambao watapimwa ikiwa wagombea hao wanastahili.
Wachambuzi wa masuala ya siasa nchini Marekani wanasema mwanamama Elizabeth Warren alifanikiwa pakubwa katika mdahalo wa hivi leo ambapo alijaribu kuzungumzia namna atakavyobadili sera za nchi hiyo kuhusu mambo ya nje na masuala ya wahamiaji.
Katika mdahalo huo wagombea karibu wote walijikita katika masuala ya msingi huku jina la rais wa Marekani Donald Trump likitajwa mara chache zaidi ukilinganisha na midahalo ya mwaka 2016.