Leo July 3, 2019 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameongoza zoezi la kumwaga dawa ya kuua vimelea vya Homa ya Dengue, katika maeneo ya Mchikichini wilayani Ilala, jijini Dar es salaam.
“Leo nimefanya ziara mkoani DSM, Ilala Manispaa ili kukagua utekelezaji wa maelekezo niliyotoa kwa Mikoa/Halmashauri ya kupambana na ugonjwa wa Dengue nchini” Waziri Ummy
“Kwa ufupi nimeridhishwa na hatua walizochukua hususani Ilala Manispaa chini ya uongozi mahiri wa DC Sophia Mjema, Mkurugenzi wa Ilala na Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu ikiwemo, kununua mashine mpya 14 za kupuliza dawa (motorised sprayers) – wamenunua viuadudu kutoka kiwandani Kibaha lita 3,980 (shs 53m) – Wamenunua lita 210 za kuua mbu wapevu na upuliziaji unaendelea ktk kata 25” Waziri Ummy
“Matokeo ya jitihada hizi yanaonekana idadi ya wagonjwa wa Dengue Wilaya ya Ilala imepungua kutoka wagonjwa 527 mwezi Mei 2019 hadi wagonjwa 207 mwezi June 2019, kwa ujumla, wagonjwa wa Dengue Mkoa wa DSM pia wamepungua kutoka 2,759 mwezi Mei 2019 hadi wagonjwa 790 mwezi June” Waziri Ummy
MIRADI SITA YA BILIONI 100 ILIVYOSAINIWA MBELE YA MAWAZIRI WAWILI