Kwa mujibu wa mtandao wa Rap Up umeripoti kuwa baada ya Mahakama Kuu nchini Sweden kutupilia mbali ombi la dhamana kuhusu kesi inayomkabili Rapper Asap Rocky, imezidi kuelezwa kuwa Asap ataendelea kubaki rumande .
Inaelezwa kuwa Mahakama hiyo imeamua kuwa Asap Rocky aendelee kushikiliwa kwa wiki mbili huku upelelezi ukiendelea wa tukio la kumpiga kijana mmoja uliotokea June 30,2019 mitaa ya Stockholm, Sweden ambapo watu watatu tayari walikuwa wamekamatwa kwa jailli ya kufanyiwa uchunguzi wa sakata hilo.
Hapo awali iliripotiwa kuwa kutokana na kesi hiyo ya kuanzisha ugomvi Asap Rocky ana uwezo wa kuhukumiwa kifungo cha miaka 6 jela akiwa nchini humo.
Audio: Amber Rutty “Kuna utofauti mkubwa kati yangu na Davil kwenye video”