Wakazi wa Kijiji cha Kangeme Kata ya Uloa Wilayani Ushetu Mkoani Shinyanga wamelalamikia baadhi ya Askari Polisi kuvujisha siri za taarifa kwa wahalifu hali inayopelekea wananchi kutotoa taarifa za kiuhalifu kwa Jeshi hilo wakihofia usalama wao. Wamezungumza hayo wakati wa Mkutano wa hadhara mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Eng. Hamad Masauni aliyeamua kufanya ziara katika kijiji hicho baada ya kukithiri kwa matukio ya kiuhalifu ikiwemo Uporwaji wa fedha,Matukio ya Ubakaji na Uvunjwaji wa Nyumba.
Baada ya kusikiliza malalamiko hayo Eng. Masauni akatoa maagizo kwa Kamanda wa Polisi mkoa pamoja na OCD kuhakikisha Wanawachukulia hatua za kinidhamu Askari wote watakaobainika kujihusisha na matendo hayo.