Baada ya Wananchi wawili pamoja na Majambazi wawili kuuawa katika mapambano ya kurushiana risasi baina ya Polisi na Majambazi katika Kijiji cha Kumtundu Kata ya Makere Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma
Wananchi wa Kijiji hicho walitaka kujua nini kifanyike juu ya kupunguza ujambazi huo kwani wengi wanaofanya matukio hayo ni wale walioajiriwa kwa ajili ya shughuli ya kilimo kutoka nchi jirani katika mashamba ambapo mchana hulima na usiku huenda kufanya ujambazi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma ACP Marti Otieno amewataka wakazi wa maeneo yote yanayoathiriwa na matukio ya ujambazi kuhakikisha yanatoa ushirikiano kwa Polisi ili kusaidia katika kufichua watu hao ambao wamekuwa wakizorotesha amani kwa wakazi hao.
Aidha katika tukio hilo Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata simu 43 zilizokuwa zimeporwa na majambazi hao pamoja na bomu moja la kutupa kwa mkono na magazine moja.