Ni miezi mitatu imepita tokea Rapper Nipsey Hussle afariki sasa imeripotiwa kuwa mtoto wa Nipsey, Kross Asghedom aliyezaa na muigizaji Lauren London atapewa kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 2 za Kitanzania kama pesa za uhifadhi ‘Guardianship’ kwenye urithi wa baba yake.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizohifadhiwa na mtandao wa The Blast umeripoti kuwa mama mzazi wa mtoto huyo Lauren London amefungua faili kwa ajili ya kuhakikisha mwanae huyo mwenye umri wa miaka miwili anakuwa na usalama na maisha yake.
Imeripotiwa kuwa kwenye faili hilo Lauren amekiri kwa kuandika kuwa kwa sasa ana jukumu la kuwalewa watoto wote aliowaacha Nipsey na anapenda kuwa mlezi wa mwanae katika kumsimamia masuala ya kisheria ikiwemo suala za mali alizoacha Nipsey na imeelezwa kuwa Lauren alimuandikisha mtoto wa kwanza wa Nipsey, Emani’10 kama ndugu wa Kross.
Mauaji ya Rapper Nipsey Hussle yaliyotokea March 31,2019 nje ya duka lake la ‘The Marathon Clothing’ mjini Los Angeles na alipumzishwa April 12,2019 katika makaburi ya Forest Lawn Memorial Park yaliyopo Hollywood Hills.
VIDEO: UWOYA KAFUNGUKA “NIKO NA MPENZI, NAKULA BATA, NINA NYUMBA MBEZI BEACH”