Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amezungumzia kuhusu takwimu za Kimataifa za Elimu ya Juu kwamba ifikapo mwaka 2017 asilimia 1 hadi 3 ya kila Watanzania Mia Moja wenye umri wa miaka 25 ndio wanapata Elimu ya Chuo Kikuu idadi ambayo ni ndogo kulinganisha na Kenya asilimia 4, Zambia 4.
“Takwimu za Kimataifa za Ushiriki wa Elimu ya Juu zinaonyeasha kwamba kufikapo mwaka 2017 asilimia 1 hadi 3 ya kila Watanzania mia moja wenye umri wa miaka 25 ndio wanapata elimu ya Chuo Kikuu idadi hii ni ndogo zaidi ya majirani zetu wa Kenya wenye asilimia 4, Zambia asilimia 4, Namibia asilimia 14” Waziri Mkuu
“Hivyo tunayo kazi kubwa ya kufanya kwa pamoja sote NACTE, TCU lakini pia na Vyuo Vikuu vyenyewe kuhakikisha tunaongeza jitihada za mikakati ya kuboresha uwiano huo ambao kwa sasa upo chini ukilinganisha na majirani zetu na kwa kweli hakuna sababu ya kuwa chini ya majirani zetu,” Waziri Mkuu