Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji imetoa ufafanuzi kuhusu Mwandishi wa kujitegemea, Erick Kabendera baada ya kusambaa kwa taarifa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kuwa amekamatwa na anahojiwa kuhusu uraia wake na Idara ya Uhamiaji Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Jijini DSM, Kamishna wa Uraia na Pasipoti wa Idara ya Uhamiaji, Gerald Kihinga, amesema kuwa Erick Kabendera ameshikiliwa na Jeshi la Polisi na Uhamiaji Jijini DSM kwa mahojiano zaidi ili kuweza kupata taarifa juu ya uraia wake.
Kamishna huyo wa Uhamiaji amesema kuwa Idara ya Uhamiaji inadhamana kubwa ya kusimamia na kutekeleza Sheria ya uraia wa Tanzania sura ya 357 rejeo la 2002, inayotoa mamlaka kwa taasisi hiyo kuchunguza na kuthibitisha uraia wa mtu yeyote.