Asubuhi ya August 3,2019 na Jumapili iliripotiwa kuwa watu wanaoishi El Paso mjini Texas Marekani pamoja na Dayton, Ohio walipata maafa makubwa baada ya kudaiwa kuwa kijana mmoja aliamua kumimina risasi na kuua watu zaidi ya 20 huku ikiripotiwa kuwa shambulio hilo ni la 250 mwaka huu.
Baadae ziliripotiwa taarifa kuwa kijana huyo aliyesabisha mauaji alitambulika kwa jina la Connor Betts mwenye umri wa miaka 24 na kuelezwa kuwa Polisi walifanikiwa kumpiga risasi kijana huyo huku akiwa amesababisha vifo vya watu 9 mjini Dayton na kuacha idadi kubwa ya watu wakiwa wamejeruhiwa.
Rais Donald Trump alitumia ukurasa wake wa Twitter kuelezea shambulio hilo ambapo mastaa mbalimbali walionekana kupinga kile ambacho alikisema Rais huyo wa Marekani. Mwimbaji Rihanna akiwa miongoni mwa mastaa waliopinga kile ambacho alikisema Donald Trump
‘Kwa hihi ambacho kimetokea leo El Paso, Texas kilikuwa sio kitu tu cha kutisha, kilikuwa ni kitendo cha kutokua na uwepo mkubwa wa kufikiri, najua nasimama na kila mtu kwenye Nchi hii anaelaani chuki ya leo. Hakuna sababu ambayo itahalalisha mauaji ya watu ambao hawana makosa”
“Donald, unaongelea “Ugaidi” Nchi yako imepatwa na matukio mawili ya Ugaidi mfululizo na kupoteza maisha ya watu 30 wasio na hatia. Hii ni baada ya siku kadhaa ya shambulio la California ambapo gaidi aliweza kununua kihalali silaha aina ya (AK-47) mjini Las Vegas, kisha akaenda kuua watu 6 kwenye tamasha moja ikiwemo mtoto mdogo wa Kiume”
“Fikiria kwenye dunia (Nchi) ambayo ni rahisi kupata AK-47 kuliko VISA! Dunia ambayo wanajenga ukuta ili kuwaacha Magaidi Marekani. Maombi yangu na rambi rambi ziende kwa familia na wapendwa wote wa majeruhi na jamii iliyoathirika toka Texas, California na Ohio! Poleni sana hakuna anayestahili kufa kama hivi.” >>> Aliandika Rihanna
VIDEO: MBASHA KAMUOA MUNALOVE? “ANANIKUBALI SANA, MI PIA NAMKUBALI”