July 5, 2019 katika Mkoa wa Mbeya mpakani mwa Wilaya ya Mbeya na Chunya katika eneo la Lwanjilo kumetokea na ajali ya basi la abiria linalofanya safari zake kati ya Mbeya kwenda Chunya na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi ambao wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya na wengine katika Hospital ya Wilaya ya Chunya.
Mpaka sasa taarifa kamili ya majeruh ni zaidi ya 19 ambao wanaendelea kupatiwa huduma
Taarifa hiyo ambayo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika ambaye alifika eneo la tukio na kwenda kuwaona wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.