Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora imemhukumu kifungo cha maisha jela Isaya Athanas (30) baada kutiwa hatiani kwa kosa la kulawiti na kubaka mtoto mwenye umri wa miaka mitano jina tunalihifadhi mkazi wa kata ya Cheyo manispaa ya Tabora.
Isaya Athanas ambaye alikuwa akifanya kazi ya kuchuga ng’ombe kwa mama mlezi wa mtoto huyo ambaye inadaiwa amekuwa akimfanyia kitendio hicho akiwa chumbani kwake kati ya January na April 2019 wakati alipogundulika.
Mapema mtuhumiwa Issaya Athanas alifikishwa mahakamani 27 April alikamatwa hapa kuja kusikilisha shitaka linalomkabili.
Akisoma hukumu katika shauri hilo namba 54 la mwaka 2019 hakimu mkazi mkoa wa Tabora Jocktan Rushwela amedai kuwa Issaya Athanas alitenda kosa hilo kati ya Januari na April 2019 kinyume na kifungu cha 130 kidogo cha (1)&(2) e na kifungu cha 131 kidogo cha 3 kanuni ya adhabu ambapo alimbaka na kumlawiti mtoto huyo.
Upande wa Jamhuri katika shauri hilo walisikiliza shahidi wanne ambao maelezo yao yalionesha Issaya Athanas amehusika kutenda unyama huo.
Hata hivyo kabla ya kutolewa adhabu mtuhumiwa Issaya Athanas alikiri kutenda kosa hilo huku akiiomba mahakama apunguziwe adhabu kwa madai shetani alimpitia.
Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora chini ya hakimu Joktani Rushwela baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili ikajiridhisha pasina shaka yoyote kwamba Issaya Athanas ametenda kosa hilo na hivyo kumuhukumu kifungo cha maisha jela.
‘YESU’ FEKI ALIETAMBA KENYA AFARIKI, WACHUNGAJI WAKAMATWA
https://youtu.be/_w-dBjGwct8