Mbunge wa Kigoma Mjini & Kiongozi wa ACTwazalendo Zitto Kabwe amerejea katika mtandao wa Twitter, baada ya akaunti yake kutokuwepo hewani kwa wiki kadhaa.
Zitto ameeleza kuwa akaunti yake ilidukuliwa baada ya kutoweka na baadaye kupatikana kwa aliyekuwa msaidizi wake.
“Walipopata access ya akaunti yangu waliweka tweets zao hizi. Tulikasirika kuwa wameingilia akaunti yangu lakini hizi ndio zilifanya tumwokoe Raphael” Zitto Kabwe
“Walitaka pia kuleta mtafaruku ndani ya chama ACTWazalendo ili kama kupunguza nguvu ya Chama katika kuhami demokrasia yetu na kuondoa udikteta unaonyemelea Nchi yetu.Nashukuru kuwa tupo imara mno ndani ya chama kwani tunajua shabaha yetu ni nini katika kuikoa Nchi yetu” Zitto Kabwe
“Chama chetu cha ACTWazalendo ndio chama kikachokua kwa kasi kuliko vyama vyote nchini hivi Sasa. Tunakaribisha kila mtu ambaye anaamini katika Tanzania yenye demokrasia ili kuwapa furaha wananchi” Zitto Kabwe
“Wamenisaidia kazi. Kila mtu na awe huru sasa” Zitto Kabwe
Tweet nyingi alizoandika Zitto Kabwe zipo kwenye Twitter yake.