Rais Magufuli ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano iliamua kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kununua vifaa vipya na vya kisasa, kuongeza wafanyakazi na kuibadili kutoka kuwa Wakala wa Serikali na kuwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kutambua umuhimu wake mkubwa na kuiongezea nguvu za kufanya kazi kwa uhuru zaidi ili kupata manufaa yanayotarajiwa.
Akizungumza katika Ofsi hiyo JPM amefichua kufariki kwa aliemuita mtani wake ambae alimdai Kitambulisho wakati anapatiwa matibabu.