Shirikisho la soka Tanzania TFF leo kupitia afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura wametangaza kufanya mabadiliko ya maboresho ya kanuni za Ligi Kuu, baadhi ya kanuni zilizofanyiwa mabadiliko katika Ligi Kuu na Ligi daraja la kwanza ni hizi.
-Wachezaji wa kigeni wanaendelea kubaki 10 na wote wanaweza kutumika kwenye mchezo mmoja.. Sharti mchezaji wa kigeni anayesajiliwa awe anacheza timu ya Taifa au Ligi Kuu ya nchi husika.. Wanaotoka Ulaya na Amerika angalau wawe wanatoka Ligi daraja la tatu au inayolingana na hiyo.
-Timu za Ligi Kuu kupungua hadi 18 msimu ujao.
-Timu nne msimu huu (2019/20) zitashuka daraja moja kwa moja yaani aliyeshika nafasi ya 17/18/19/20 anashuka moja kwa moja kwenda ligi daraja la kwanza huku aliyeshika nafasi ya 15/16 atacheza Play Off na timu za ligi daraja la kwanza.
-Msimu wa 2020/21 ligi kuu itashirikisha timu 18 ikiwa timu 14 zilizobaki ligi kuu, timu 2 ambazo zimepanda daraja moja kwa moja kutoka ligi daraja la kwanza na timu 2 washindi wa jumla wa Play Off ya timu zilizoshika nafasi ya 15/16 ligi kuu na washindi wa wa jumla wa Play Off ya ligi daraja la kwanza.
-Kuanzia msimu ujao makocha wa timu za TPL watapaswa kuwa na leseni A ya CAF au inayolingana na hiyo.
-Kocha akionyeshwa kadi nyekundu atakosa mechi tatu na hataruhusiwa kuingia hata kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Atatozwa faini ya laki tano pia.
VIDEO: Kwa tathmini hii ya Edo Kumwembe, Mashabiki wa Chelsea haina budi kuwa wavumilivu