Leo August 28, 2019 Kundi la Watanzania limejitokeza leo nje ya Ubalozi wa Afrika Kusini uliopo jijini DSM likishinikiza kuachiwa kwa ndege ya Air Tanzania inayoshikiliwa nchini Afrika Kusini.
Ndege hiyo inashikiliwa kwa siku tano zilizopita kutokana na kesi ya kudai fidia inayomhusu Hermanus Steyn, raia wa Afrika Kusini dhidi ya Serikali ya Tanzania
Watu hao waliokusanyika nje ya Ubalozi huo wameonekana wamebeba mabango mbalimbali huku wakiimba “Tunataka ndege yetu”.