Raia kadhaa wa Afrika Ya Kusini wanaoishi katika Jiji la Johannesburg wamechoma moto na kuiba Bidhaa katika Maduka ya raia wakigeni waishio katika Mji huo.
Hata hivyo hali hii imeendelea kutokea kwa raia wa kigeni ambao inasemekana wanawanyima ajira raia wazawa wa Afrika ya Kusini na imesababisha mzozo mkubwa kati ya Waafrika Kusini na raia wa kigeni ambao wanafanya biashara mbalimbali Nchini humo.
Katika Hatua Nyingine Waziri wa Mambo ya nje wa Nigeria Geoffrey Onyeama ametoa Neno kupitia ukurasa wake wa Twitter nakusema kuwa maduka ya raia wa Nigeria yalilengwa na “wahalifu wasio na akili” na akaahidi kuchukua “hatua dhahiri”. Maeneo yaliadhiriwa hapo jana na vurugu hiyo ni Jeppestown, Denver, Malvern na Tembisa.
Baadhi ya taarifa kutoka nchinihumo zinaeleza Watu 41 wamekamatwa na Polisi nchini Afrika kusini kwa madai ya kupora mali na kuchoma maduka ya Wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika.