Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amewataka Watanzania kuondoa wasi wasi kuhusu mijadala inayoendelea mitandaoni kuhusu ujenzi wa Bomba la Mafuta na Gesi baina ya Tanzania na Uganda.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Waziri Bashungwa amesema “Nilizungumzie suala hili kama ifuatavyo katika industries ya Oil and Gas mambo ya kitalu aliyekuwa sehemu ya kitalu kuingia na kutoka ni jambo la kawaida, kwahiyo yanayoendelea kule Uganda kwamba huyu anataka kuingia huyu anataka kutoka ni jambo la kawaida,”
Pia amesema kuwa “Lakini kama mnavyofatilia bado hatujapata officials position kama yanayozungumziwa kwenye mitandao ni kweli ama lah kwahiyo siwezi kulizungumzia maana kuna a lot on the air,”
“Kwahiyo tusubiri kwa sababu tuna vikao vya mawaziri wa Tanzania na Uganda na mimi nitashiriki hivyo mambo haya tutayajadili kisha tutakuwa na position ya kuliongelea, lakini niwaondoe wasi wasi kwenye suala hilo katika mijadala inayozunguka ni jambo la kawaida,” Bashungwa