Mkali kutokea bongoflevani Madee Ally amepiga marufuku kwa nyimbo zake alizowahi kushoot kwenye ardhi ya Afrika Kusini kuendelea kuchezwa kwenye vituo vya television akiamini kuendelea kuzipiga ni kunadi ardhi ya watu ambao wamekuwa wakiwatenga wa Afrika wenzao.
Madee ameeleza sababu zaidi ya mbili za yeye kupiga marufuku hiyo kwa kutaja machafuko yanayoendelea nchini humo juu ya raia wa kigeni haswa wakiafrika na pia amefanya hivyo ili kumuenzi rais mstaafu wa Zimbabwe mzee Mubage aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Madee ameongeza kwa kusema ameamua kuchukua uamuzi wa kufuta video zake kwenye channel yake ya YouTube na kusema hayuko tayari kuendelea kuitangaza Afrika kusini kupitia muziki wake.
Madee kaandika….>>>>“Mambo vipi naitwa MadeeAlly leo Sept 06 2019 kwa hiari yangu nimeamua kuzuia kuchezwa kwa nyimbo zangu ambazo nimezifanya kwenye ardhi ya South Africa especially #VUVULA na zingine zisipigwe kwenye kituo chochote cha habari na zaidi ikiwa ni ni TV, Kwa sababu TV ndio kitu kinachoonyesha mandhari ya nchi tajwa ambayo ni SA, Binafsi nimechukua hatua kwanza kwa kuufuta hata kwenye channel yangu ya Youtube ambako ulikua unapatikana.
Binafsi wakati natoka Manzese kwenda kushoot SA plan ilikua nikutangaza vivutio vya Africa kwa ujumla, Kwa kuwa imani inaniambia sisi Waafrika ni Wamoja.
Nimefikia hatua hii kwa sababu kuu mbili.. (1)kile kinachoendelea kwasasa kila mtu anajua namna Wasouth Africa wanachowafanyia Waafrika wenzetu, 2) Ni kumuenzi Mzee wetu MUGABE ambae wengi wetu humu tunajua historia yake ya kupambania mtu mweusi (Mwafrika)na miongoni mwa watu waliokua wakipinga utawala wa watu weupe alikua anapambana kuhakikisha Waafrika tunajikomboa.
Sitakua sawa kuendelea kuitangaza SA kupitia muziki wangu, ZIMA KWAITO 🎤❎ R.I.P ROBY”