Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewakuta na kesi ya kujibu viongozi 9 CHADEMA, akiweko Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe ambapo wanapaswa kuanza kujitetea Septemba 17, 18 na 19, mwaka huu.
Washitakiwa hao wamekutwa na kesi ya kujibu leo baada ya upande wa mashitaka kufunga ushahidi wao.
Awali, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa mashahidi nane wanatosha kuthibitisha kesi yenye mashitaka 13 yanayowakabili washitakiwa hao hivyo wanafunga ushahidi dhidi ya kesi hiyo.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba alisema washitakiwa wote wanakesi ya kujibu kama wanavyokabiliwa na mashitaka katika mahakama hiyo ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 17,18 na 19 mwaka huu.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari Mosi na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.
Mbali ya Mbowe washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu Taifa, Dk Vincent Mashinji , Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.
Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.
NAPE ATINGA KWA MIGUU IKULU KUOMBA ASAMEHEWE “SINA AMANI, NAKOSA USINGIZI “