Leo September 19, 2019 Msanii wa muziki na mfanyabiashara nchini Kenya, Akothee amekutana na kizuizi cha walinzi katika eneo la majengo ya Bunge kutokana na aina ya mavazi yake aliyovaa
Akothee alifika Bungeni hapo kwa mwaliko wa Mbunge David Sankok, alizuiwa kwa takribani dakika 20, baadae aliruhusiwa kuingia katika Mgahawa wa eneo la Bunge baada ya kujistiri kwa mtandio aliopewa na Afisa mwanamke aliyekuwa katika eneo hilo.
Hata hivyo, Akothee alisikika akisisitiza juu ya mavazi yake kuwa ndo uvaaji wake tofauti na alivyotakiwa kuvaa ili aweze kuingia eneo hilo.