Leo September 19, 2019 Wakala wa Serikali na kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Airbus wamesaini mkataba wa ununuaji wa ndege mbili aina ya Airbus A220-300 ambazo zitatumiwa na Shirika la ndege la Tanzania (ATCL).
Mkataba huo umesainiwa leo ambapo Airbus imewakilishwa na Makamu wa rais wa kampuni hiyo Afrika, Hadi Akoum na upande wa Serikali alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Ndege za Serikali, Benjamin Ndimila.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo, Ndimila ambaye hakutaja gharama halisi inayotumika kununua ndege hizo amesema ndege hizo zitakuwa na tofauti na za aina hiyo ambayo tayari zinatumiwa na ATCL kwani kila kiti kitakuwa na ‘skrini’ “jambo hii ni historia inaacha historia”.
“JAMBAZI TUTAENDA NAE KIJAMBANZI, UGOMVI WETU NI KWA WANAOTUFANYIA NDIVYO SIVYO” RC KIGOMA