Leo September 24, 2019 Serikali imemwita Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa nchini kupata kwa kina hoja za Shirika hilo zinazosambaa kupitia vyombo vya habari.
Mwakilishi huyo amesisitiza kuwa WHO haijasema wala haina ushahidi wowote kuwa Tanzania kuna Ebola na itashirikiana na Serikali.
Aidha, katika mazungumzo hayo WHO imeafiki kuwa kama kuna mahitaji ya kupata taarifa zaidi kutoka Serikali ya Tanzania lazima utaratibu ulioanishwa katika miongozo ya taasisi hiyo na ambayo imeridhiwa na Serikali ifuatwe kikamilifu.