Club ya Azam FC kwa sasa ipo Harare nchini Zimbabwe kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Triangle FC, mchezo ambao utachezwa katika uwanja wa Bulawayo chini Zimbabwe siku ya.
Mchezo huo ambao ni muhimu kwa Azam FC kupata ushindi kwa namna yoyote au unaweza kusema ni mchezo wa kufa na kupona, Azam FC imewasili na wachezaji wake wakiwa fiti sambamba na viongozi wao wakuu wameingia leo kuiongezea nguvu akiwemo CEO wao Abdulharim ‘Popat’
Hata hivyo afisa habari wa Azam FC Jafari Iddi Maganga aliyethibitisha ujio wa viongozi hao, leo ameripoti kuwa ndio kwa mara ya kwanza mvua imenyesha na baridi kali, unaambiwa kwa miaka miwili Zimbabwe ilikuwa haijapata mvua kunyesha, hivyo kwa imani za kiafrika wanatafsiri kuwa Azam FC imekuja na baraka.
VIDEO: Antonio Nugaz kaanza na Mbwembwe Yanga “Yanga unyonge kwisha”