Kichaa cha Mbwa ni ugonjwa ulioathiri maeneo mbalimbali nchini Tanzania na maeneo mengine duniani, hususan bara la Asia na Afrika, ugonjwa huu unasababishwa na virusi jamii ya ‘lyssa’ ambavyo hukaa katika mate ya wanyama jamii ya mbwa walioathirika (mbwa, paka, mbweha, fisi na wengineo).
Binadamu hupata maambukizi pale anapoumwa na mnyama aliyeathirika, ambapo virusi huingia kupitia jeraha analopata. Takwimu zimekadiria kuwa ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa husababisha takribani vifo 59,000 kila mwaka duniani, ambapo kati ya vifo hivyo, asilimia 36 hutokea katika bara la Afrika.
Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 30 hadi 50 ya waathirika wa kichaa cha mbwa ni watoto chini ya miaka kumi na tano. Ugonjwa wa kichaa cha mbwa hauna tiba.
MAGUFULI ATOA ONYO “DPP WANAOSHIKWA SAIVI USISAMEHE, SIFANYI KAZI YA KITOTO”