Kampeni ya Matibabu ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto 10 kutoka familia duni kila mwezi kwa Muda wa Miezi 6 iliyoanzisha na Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda imeendelea kuleta matokeo chanya na kuokoa Maisha ya Watoto ambapo
Leo September 30 Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy imemkabidhi Mkuu huyo wa Mkoa hundi ya shilingi Milioni 40 ikiwa ni sehemu ya Kuunga mkono kampeni hiyo.
Akipokea hundi hiyo RC Makonda amesema kiasi hicho cha fedha kitasaidia kuokoa maisha ya takribani watoto 20 kutoka familia Duni ambao wamelazwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wakisumbuliwa na tatizo la moyo lakini wameshindwa kupata matibabu kutokana na kushindwa kumudu gharama.
MAGUFULI ATOA ONYO “DPP WANAOSHIKWA SAIVI USISAMEHE, SIFANYI KAZI YA KITOTO”