Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayekipiga katika club ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji Mbwana Samatta amefunguka na kueleza kiu ya watanzania kuelekea mchezo wao wa UEFA Champions League dhidi ya Liverpool huo ukiwa ndio mchezo wao wa tatu wa hatua ya Makundi.
Samatta kuelekea mchezo huo akiambatana na kocha wake mkuu Felice Mazzu aliongea na vyombo vya habari, huku Samatta akieleza kuwa zamani alikuwa shabiki mkubwa wa Man United na anafahamu kuwa Tanzania wanashauku ya kuona akicheza dhidi ya Virgil van Dijk na kumpita.
“Nilipokuwa mdogo nilikuwa shabiki wa Man United lakini kwa sasa hatuizungumzii Manchester, tunaizungumzia Liverpool tunacheza mbele ya mashabiki wetu na tunataka kufurahia mwisho wa game tutajitahidi kadri ya uwezo wetu, hii ni mechi ya ndoto wakati unapocheza mpira unaota kucheza mechi kama hizi”>>>Samatta
“Kila mtu Tanzania anazungumzia kuhusiana na mechi ya kesho (October 23) anazungumzia kuhusiana na Samatta na Van Dijk, wanasema natakiwa kufanya kitu dhidi ya Virgil Van Dijk, nafikiri wengi wao wataangalia mechi hapo kesho”>>>>Samatta
KRC Genk wapo nafasi ya mwisho wakiwa na point moja katika msimamo wa Kundi lao E lenye timu za Napoli ya Italia anayeongoza kwa point 4, Liverpool ya England aliye nafasi ya tatu kwa kuwa na point 3 sawa na RB Salzburg ya Austria aliye nafasi ya pili kwa kuwa na point 3 akimzidi Liverpool tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.
AUDIO: SERGIO AGUERO WA MAN CITY AMEPATA AJALI