Usiku wa October 23 ulikuwa usiku wa kihistoria kwa mtanzania Mbwana Samatta kwani alikuwa anacheza dhidi ya Liverpool Samatta akiwa ndio nahodha wa KRC Genk katika mchezo huo wa UEFA Champions League.
Kiu ya watanzania wengi walikuwa wanatamani kuona Mbwana Samatta akifunga goli dhidi ya Liverpool iliyokuwa chini ya safu ya ulinzi mkali wa Virgil van Dijk katika uwanja wa Luminus.
Mchezo huo kwa bahati mbaya ulimalizika kwa Genk kupoteza 4-1 huku mtanzania Mbwana Samatta goli alilofunga likikataliwa na refa mchezo huo Slavko Vincic baada ya kuangalia VAR na kudai kuwa aliotea licha.
Magoli ya Liverpool yalifungwa na Chamberlain dakika ya 2 na 57, Sadio Mane dakika ya 77 na Mo Salah dakika ya 86, huku la Genk likifungwa na Odey dakika ya 88, Samatta anaacha historia vichwani mwa watanzania kwa kuwa mtanzania wa kwanza kucheza dhidi ya Liverpool huku akipewa dhamana ya unahodha.
AUDIO: SERGIO AGUERO WA MAN CITY AMEPATA AJALI